1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
  • Uganda: Uhuru baada ya miaka 66

    Uganda- Miaka 50 ya Uhuru

    Uganda: Uhuru baada ya miaka 66

    Oktoba 9 mwaka 1962 Uganda ilipata uhuru kutoka kwa Uingereza (kushoto-kulia): Gavana Walter Coutts, waziri mkuu Milton Obote, Katharine Herzogin von Kent na Edward Herzog von Kent siku moja kabla uhuru.

  • Milton Obote

    Uganda- Miaka 50 ya Uhuru

    Milton Obote

    Baada ya kupata uhuru kutoka kwa Uingereza Milton Obote alikuwa waziri mkuu wa kwanza wa Uganda. Aliufuta utawala wa kifalme. Obote alikuwa rais mwaka 1966 hadi mkuu wa majeshi Idi Amin alipompindua Januari 25, 1971. Kupitia uchakachuliwaji wa kura Obote alirudi madarakani mwaka 1980. Awamu hii ya pili ya uongozi wake iligubigwa na ukandamizaji, maelfu ya watu kuuwawa na kuyakimbia makazi yao.

  • Idi Amin

    Uganda- Miaka 50 ya Uhuru

    Idi Amin

    Wakati wa utawala wake wa kiimla kuanzia mwaka 1971 hadi 1979 malefu ya watu walikamatwa, kuteswa na kuuwawa. Aliwafanya wapinzani wake wa kisiasa kuwa chakula cha mamba au kuwalazimisha wapigane kutumia nyundo. Raia wa Asia walipokonywa mali zao na kufukuzwa nchini. Amin aliaga dunia mwaka 2003 akiwa uhamishoni nchini Saudi Arabia.

  • Ukombozi wa Uganda

    Uganda- Miaka 50 ya Uhuru

    Ukombozi wa Uganda

    Msaada ulikuja Aprili mwaka 1979 kutoka nchi jirani ya Tanzania. Majeshi ya Tanzania pamoja na raia wa Uganda waliokuwa uhamishoni yalimshinda Idi Amin na kumaliza miaka minane ya utawala wa umwagaji damu. Katika uchaguzi wa mwaka 1980 Milton Obote alishinda tena. Yoweri Museveni alipigania kuingia madarakani mwaka 1986 na leo ni rais wa Uganda.

  • Uganda- Miaka 50 ya Uhuru

    "Lulu ya Afrika"

    "Lulu ya Afrika" ndivyo alivyoiita Winston Churchhill nchi hiyo ya Afrika Mashariki isiyo na bahari na yenye mandhari yake mazuri: kijani kibichi na maziwa, misitu na milima. Mazao yaliyokuwa kutokana na hali nzuri ya hewa ni ndizi, miwa, pamba na hasa kahawa kwa kuuzwa nje ya nchi.

  • Joseph Kony

    Uganda- Miaka 50 ya Uhuru

    Joseph Kony

    Ni mhalifu wa kivita anayetafutwa sana. Kony alifanya ugaidi kwa zaidi ya miaka 20 kaskazini mwa Uganda na kundi lake la Lords' Resistance Army (LRA). Kundi la LRA liliwateka nyara na kuwasajili kwa nguvu watoto wapatao 20,000. Baada ya kusambaratika mkataba wa amani wa mwaka 2008 amekuwa akiwahangaisha watu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

  • Kizza Besigye

    Uganda- Miaka 50 ya Uhuru

    Kizza Besigye

    Kiongozi wa upinzani na kiongozi wa chama cha Forum for Democratic Change (FDC) aliyepoteza chaguzi kadhaa. Sera zake za chama haziuvutii umma wa Uganda na hajafaulu kuunganisha pamoja upinzani. Tangu Septemba mwaka 2011 anaongoza maandamano ya kutembea kwenda kazini dhidi ya bei za juu za chakula na kukosekana haki katika jamii.

  • Machafuko kupitia vyombo vya Usalama

    Uganda- Miaka 50 ya Uhuru

    Machafuko kupitia vyombo vya Usalama

    Mara kwa mara maandamano ya amani huzimwa na vyombo vya usalama vya Uganda kutumia nguvu na ukamataji watu usio na maana. Wanaharakati wanadai polisi na makundi ya kijeshi hayafikishwi mbele ya vyombo vya sheria kwa uvunjaji wa haki za binaadamu.

  • Ubaguzi dhidi ya Ushoga na Usagaji

    Uganda- Miaka 50 ya Uhuru

    Ubaguzi dhidi ya Ushoga na Usagaji

    Ushoga umeenea sana Uganda. Mwaka 2011 gazeti moja lilichapisha picha zenye majina na anwani za mashoga na wasagaji. Baadaye kulianza kampeni ya kisheria dhidi ya watu hao. Nchini Uganda ndiko kwenye sheria kali kabisa dhidi ya mashoga na wasagaji ambazo zimekosolewa na Umoja wa Ulaya na Marekani.

  • Amisom

    Uganda- Miaka 50 ya Uhuru

    Amisom

    Tangu miaka kadhaa wanajeshi wa Uganda wanapigana nchini Somalia upande wa serikali ya nchi hiyo. Wanajeshi hao ni sehemu kubwa ya kikosi cha amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia. Tangia hapo Uganda ikalengwa mara kadhaa na mashambulio ya wanamgambo wa al Shabaab kutoka Somalia.

  • Chaguzi mwaka 2011

    Uganda- Miaka 50 ya Uhuru

    Chaguzi mwaka 2011

    Huru lakini si haki, ndiyo iliyokuwa tathmini ya waangalizi wa chaguzi za mwaka 2011. Rais wa Uganda Yoweri Museveni (kushoto) alijihakikishia uungwaji mkono na idadi kubwa ya wananchi kupitia zawadi ya kura na kampeni za gharama kubwa. Mwaka 2005 aliibadilisha katiba ili agombee tena urais.

  • Utalii

    Uganda- Miaka 50 ya Uhuru

    Utalii

    Chanzo cha Mto Nile, mandhari ya milima na hifadhi za misitu na hivyo kutoa uwezo wa kuwaona nyani na sokwe mtu wanaokabiliwa na kitisho cha kuangamia, vinaifanya Uganda kuwa kivutio muhimu cha watalii. Mwaka 2012 Uganda iliongoza orodha ya nchi zinazowavutia watalii iliyotolewa na shirika la safari za kitalii la Lonely Planet.

  • Rais Yoweri Museveni

    Uganda- Miaka 50 ya Uhuru

    Rais Yoweri Museveni

    Kwanza alikuwa mkosoaji wa marais wa Afrika waliobakia madarakani kwa muda mrefu, lakini wakati huu ana ndoto ya kubakia rais milele. Ni jinamizi kwa idadi kubwa ya vijana ambao hawamjui rais mwingine. Museveni amekuwa madarakani tangu miaka 26 iliyopita.


    Mwandishi: A.Schmidt | Mhariri: J. Charo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.de.