1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
DW Sprachkurse Deutsch warum nicht Brandingbanner Deutsche Welle, Sprachkurse/Bildungsprogramme, (c) DW Auslandsmarketing 2012, Benutzung nur für Deutschkurse!

Deutsch – warum nicht?

Fungu 1

Andreas anafanya kazi kwenye Hotel Europa iliyoko katika mji wa Aachen ili apate kugharamia masomo yake ya uandishi habari. Vituko vinaanza baada ya kutoweka kwa mwanamuziki maarufu kutoka chumba nambari 10. Mambo muhimu ya sarufi: Mnyambuliko wa vitenzi, viwakilishi-nafsi, maswali mepesi, uhusika wa moja kwa moja.

Fungu 2

Andreas ana shughuli nyingi za kufanya. Inambidi kushughulikia wageni hotelini, kuwatafutia wazazi wake chumba na pia kumhoji Charlemagne. Ziada ya hayo, wazazi wake wanamchunguza ex ni nani na wapi alikutana na binti yao. Mambo muhimu ya sarufi: Vitenzi vya utaratibu, wakati timilifu, uhusika usioungwa moja kwa moja.

Fungu 3

Andreas bado anafanya kazi Aachen, lakini Dr Thürmann amepata kazi mpya kwa mwenye mtizamo wa kuwa mwandishi habari. Berlin: Jiji kubwa na linalovutia zaidi linamsubiri. Mambo muhimu ya sarufi: Wakati uliopita hali ya kuendelea, vishazi tegemezi, kubadilika kwa vivumishi.

Fungu 4

Andreas amekamilisha masomo yake na yuko tayari kufanya utafiti wa makala yake ya kwanza. Kazi yake inamwelekeza na inampeleka (bila shaka pamoja na rafiki yake wa ajabu ex) katika iliyokuwa Ujerumani ya Mashariki. Mambo muhimu ya sarufi: Kauli-tendwa, vishazi tegemezi, vitenzi vya kujirejea, dhamira tegemezi.

Kwa Wanafunzi

Deutsch – warum nicht?

Kozi ya Deutsch-warum nicht? iliyogawanywa katika sehemu nne, inazungumzia kisa cha mwanafunzi wa uandishi habari Andreas na rafikiye asiyeonekana ex. Ungana nao wawili hawa ujifunze Kijerumani. Miongoni mwa sehemu hizo nne, kila sehemu ina masomo 26 yaliyo na mazungumzo, mazoezi na vijalada vya kusikiliza ambavyo unaweza kuvinakili. Kozi hii inashughulikia viwango vya A1 na B1 vya Tathmini ya Ulaya ya Ujuzi wa Lugha na linawalenga wanafunzi wanaoanza kujifunza lugha na pia wale wa kiwango cha juu. Somo la Deutsch-warum nicht? lilitayarishwa na Deutsche Welle pamoja na Taasisi ya Goethe.