Mjumbe wa kimataifa nchini Syria Lakhdar Brahimi amedokeza leo(24.10.2012)kuwa pande zinazohusika katika mzozo nchini Syria huenda zikakubaliana kusitisha mapigano katika wakati wa sikukuu ya Waislamu ya Idd el Hajj.
Hali ya kaskazini mwa Mali ni ya hatari, kiasi kwamba, bila ya msaada wa jumuiya ya kimataifa haiwezi kudhibitika tena.Na uwezekano wa nchi za Afrika magharibi kujiingiza kijeshi katika nchi hiyo unazidi kuwa mkubwa
Waasi nchini Syria wanaendelea na mapambano kuiteka kambi ya kijeshi ya Wadi al-Daif iliyoko karibu na njia kuu ya kutoka kaskazini kuelekea kusini ambayo ni muhimu kwa waasi hao kudhibiti kabisaa sehemu ya kaskazini
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Cathrine Ashton amefanya ziara nchini Lebanon na kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa nchi hiyo Najib Mikati, yaliyogubikwa na Syria na mauaji ya mkuu wa upelelezi Wissam Hassan.
Kwa mara nyengine tena Rais Barack Obama ametajwa kumbwaga Mitt Romney katika mdahalo wa televisheni, ambao licha ya mada yake kuu kuwa siasa, masuala muhimu kwa wapiga kura, yaani uchumi na ajira, yalitawala mjadala.
Kundi la waasi la M23 katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, linaloshutumiwa kuzusha vurugu mashariki mwa nchi hiyo, limesema limebadili jina la tawi lake la kijeshi na linajiandaa kuzima mashambulio mapya dhidi yake.
Polisi Lebanon wamepambana na waandamanaji wakati wakijaribu kuivamia ofisi ya waziri mkuu mjini Beirut huku kukiwa na wito wa kumtaka ajiuzulu baada ya mripuko wa bomu kwenye gari kumuuwa afisa mwandamizi wa usalama.
Mjumbe wa amani wa kimataifa nchini Syria Lakhdar Brahimi Jumamosi (20.10.2012) amesisitiza mjini Damascus haja ya kusitisha mapigano, ili kuzuwia umwagikaji zaidi wa damu nchini nchini humo.
Rais wa mali Dioncounda Traore amesema kuwa, sekunde moja haipaswi kupotezwa katika kulikamata eneo la kaskazini mwa nchi hiyo kutoka kwa waasi wa Kiislamu ,wakati mkutano na viongozi wa mataifa ya Afrika na Ulaya.
Katika siku za karibuni, vyombo vinavyopaswa kulinda usalama nchini Tanzania vimekuwa vikilaumiwa kwa kujihusisha kwenye vitendo vya kuuvunja huo usalama wenyewe.
Tembelea DW katika Facebook
Tembelea DW katika Twitter
Pata huduma zetu kupitia za SMS, RSS, Kijarida na huduma nyengine za mtandaoni kutoka DW.