Ghasia zilizozuka baina ya mashabiki wa Borussia Dortmund na Schalke 04 katika mchuano wa 141 wa uhasimu wa eneo la Ruhr, ndizo zilizokuwa mbaya zaidi kuwahi kushudiwa katika miaka mingi.
Ligi ya Bundesliga inarejea uwanjani,huku mashabiki wakielekeza macho na masikio yao katika mchezo wa watani wa jadi ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa kati ya mabingwa watetezi Dortmund na mahasimu wao wa jadi Schalke.
Timu 15 zitakazojiunga na wenyeji Afrika Kusini kwa awamu ya 19 ya dimba la mataifa ya bara la Afrika zimejulikana baada ya wikendi ya mechi za kufuzu zilizojaa sarakasi na kusababisha furaha na majonzi kote barani humo
Ushindi mkubwa wa magoli sita kwa sifuri wa Ujerumani dhidi ya Ireland katika mchuano wa kufuzu kwa fainali za kombe la dunia ulirejesha utulivu ndani ya kikosi hicho, tangu dimba la UEFA EURO 2012 mwezi Juni.
Ujerumani ilijitupa dimbani Ijumaa(12.10.2012)dhidi ya Ireland ambapo wachezaji walivaa kitambaa cheusi mkononi kwa heshima ya mwanasoka wa zamani wa Ujerumani Helmut Haller aliyefariki Alhamisi akiwa na umri wa miaka 78
Mabingwa watetezi Borussia Dortmund waambulia sare na Hannover 96 ,wakati Bayern Munich yazidi kuchanja mbuga. Messi na Ronaldo ngoma droo katika el classico uwanjani Nou Camp mjini Madrid.
Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.de.
Washirika Wetu
Pata huduma zetu kupitia za SMS, RSS, Kijarida na huduma nyengine za mtandaoni kutoka DW.
Kijarida cha Deutsche Welle
Unaweza kujiunga moja kwa moja na huduma ya kupokea kijarida cha Deutsche Welle kupitia mtandao kwa kubonyeza hapa na upate taarifa za kila siku.